September 11, 2022
Chama cha Kiswahili cha Kiseryan ni chama kinachohusu lugha ya Kiswahili. Kilianzishwa mwaka wa 2015 na kinaendelea kunawiri kila kuchao kwa kile kinachofanywa na wanachama wa chama hicho.
Chama cha Kiswahili kinahusu uzungumzaji wa lugha yetu tukufu ya Kiswahili miongoni mwa wanachama wetu iliwaweze kukikuza na kuwa bora, kwa uandikaji wa insha za Kiswahili, kushiriki katika mijadala ,kujihusisha katika uanahabari ambapo wanachama wetu kuhariri habari mbalimbali na kuzisoma kwa wanafunzi wenzao na kuwapasha kwa habari zinazojiri, kushiriki katika mashindano ya Kiswahili ambayo imewasaidia wanafunzi wengi kuipenda lugha yetu.
Mbali na wanachama, pia chama hiki kimeweza kubarikiwa kuwapata walimu ambao wametoa usaidizi wao na pia kujitolea kuona chama hiki kinaendelea. Ni furaha yao kuwaona wanafunzi kuichukulia lugha ya Kiswahili kama lugha rahisi na pia kupewa nafasi kama lugha nyingine zinazoheshimiwa.
Wanafunzi na shule kwa jumla wanahimizwa kujiunga na chama hiki ili lugha ya Kiswahili iweze kuendelezwa na kupendwa na wote.Si kwa kuizungumza tu, bali hata darasani na katika jamii kwa jumla.